Wakati zikiwa zimesalia siku nne kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa, mabosi wa Yanga wanajadili wachezaji ambao wanapaswa kupunguzwa kikosini ili kuweza kusajili wapya
Yanga imekamilisha idadi ya wachezaji 12 wa kigeni na hivyo ili kuweza kusajili wapya, lazima wengine wapunguzwe
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha kuwa wako katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa wachezaji wawili wa Kimataifa ambao wanatajwa kuwa ni mshambuliaji na mlinzi wa kati
Lakini pia washambuliaji Yacouba Songne na Lazarus Kambole nao walishiriki michuano ya kombe la Mapinduzi na pengine mmoja kati yao anaweza kurejeshwa kikosini
Yanga inahitaji kuwaondoa angalau wachezaji watatu ili nafasi zao zitumike kusajili wapya
Kama mabosi wataamua kuwapunguza wachezaji kwa kuangalia mchango wao kwenye kikosi msimu huu, mchakato unaweza kuwa hivi;
Wachezaji Djigui Diarra, Yannick Bangala, Stephane Aziz Ki, Jesus Moloko, Joyce Lomalisa, Khalid Aucho na Fiston Mayele wamekuwa na mchango mkubwa kikosini msimu huu hivyo wana uhakika kwa asilimia 100 hawataguswa
Beki Djuma Shabani alianza vyema msimu lakini baadae akapoteza namba kwenye kikosi cha kwanza mbele ya Kibwana Shomari
Djuma amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara na wakati mwingine akisumbuliwa na maradhi
Winga Bernard Morrison amekuwa na mchango mkubwa lakini ni mchezaji aliyekosa mechi nyingi kutokana na majeraha au matatizo ya kifamilia
Wachezaji wengine Tuisila Kisinda na Gael Bigirimana wamekuwa na mchango wa wastani pale walipohitajika huku Heritier Makambo akiwa mchezaji aliyeonekana dimbani mara chache zaidi miongoni mwa wachezaji wa kigeni