Mkurugenzi wa Sheria klabu ya Yanga Simon Patrick ambaye aliongoza jopo la Wanasheria wa Yanga kushinda kesi ya mkataba dhidi ya Feisal Salum, ameeleza kushangazwa na vitendo vinavyofanywa na Wanasheria wa Feisal baada ya maamuzi ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF dhidi ya mteja wao
Simon amaaleza kushangazwa na Wanasheria hao kuzunguuka kwenye vyombo vya habari kupinga maamuzi ya Kamati huku wakitafuta huruma kutoka kwenye jamii
Amesema kama hawakuridhishwa na maamuzi ya Kamati walipaswa kufuata utaratibu wa kuitafuta haki ambayo wanaamini wamenyimwa na sio kutafuta huruma kwenye vyombo vya habari
ADVERTISE HERE