Mshambuliaji Yacouba Songne amewaaga Wanachama na Mashabiki wa Yanga, akiwashukuru kwa ushirikiano aliopata katika muda wote alioitumikia Yanga
Licha ya awali kuwa na matumaini makubwa ya kurejea kikosini baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa takribani miezi 12, imekuwa sio rahisi kwake kurejeshwa kikosini kutokana na ufinyu wa nafasi
Yanga imelazimika kufanya maamuzi magumu katika dirisha hili dogo la usajili ambalo litafungwa kesho Jumapili, Januari 15
Yanga imekamilisha idadi ya wachezaji 12 wa kigeni, ili kuongeza wapya inapaswa kupunguza wengine
Tayari wamemsajili mshambuliaji Kennedy Musonda ambaye anatajwa kuchukua nafasi ya mshambuliaji Heritier Makambo
Hata hivyo Yanga pia inatajwa kusajili beki mwingine wa kati ambaye huenda akachukua nafasi ya mchezaji mwingine mmoja
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ni kama ameridhishwa na wachezaji alionao pamoja na maboresho yaliyofanywa kwenye dirisha hili
Ni wazi pia mshambuliaji Lazarus Kambole naye hataweza kujumuishwa kwenye kikosi