Dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufungwa leo saa 5:59 usiku. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesisitiza hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya dirisha kufungwa
Klabu zimetakiwa kukamilisha usajili pamoja na UHAMISHO wa Kimataifa kwa wachezaji wanaotoka nje ya nchi
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga katika dirisha hili wamekamilisha usajili wa wachezaji wawili kiungo Mudathir Yahya na mshambuliaji Kennedy Musonda. Hata hivyo bado kuna utambulisho wa mchezaji mmoja unasubiriwa
Kulingana na Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe ambaye alibainisha kuwa watafunga dirisha la usajili kwa kutambulisha wachezaji wawili wa Kimataifa, ambao ni mshambuliaji (Musonda) na mlinzi wa kati
Pengine kabla ya dirisha kufungwa saa 5:59 usiku, beki huyo anaweza kutambulishwa