Kesho Jumatatu Januari 16 2023, mabingwa wa nchi Yanga watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Ihefu Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki wa timu hiyo kuhakikisha wananua tiketi zao mapema ili kuwa mashuhuda wa mchezo huo wa kisasi
Hii ni mechi ya kisasi kwa sababu Ihefu Fc waliifunga Yanga mabao 2-1 timu hizo zilipochuana kule Mbarari, Mbeya
Yanga itahitaji kudhihirisha kuwa walipoteza mchezo wa kwanza kwa bahati mbaya na wanazihitaji alama zote tatu ili waendelee kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi
Tiketi za mchezo huo zimeanza kuuzwa mapema tu ambapo viingilio VIp A ni Tsh 15,000/-, VIB B na C ni Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-


ADVERTISE HERE