Jana washambuliaji Fiston Mayele na Kennedy Musonda walicheza pamoja kwa takribani dakika 30 za mwisho za mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc ambao Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0
Bao hilo lilipatikana muda mfupi tu baada ya Musonda kuingia kucheza mechi yake ya kwanza ya ligi kuu ya NBC ikiwa ni siku moja tu tangu atue pale Avic Town
Muda mchache waliocheza pamoja, washambuliaji hao walionyesha hatari yao mbele ya lango la Ihefu Fc
Wote wana kasi, wote wana nguvu na wote wana kiu ya kufunga mabao. Zilikuwa dakika 30 ngumu sana kwa walinzi ya Ihefu Fc kupambana na washambuliaji hawa
Sasa kuna timu zitakutana na 'shughuli' ya Mayele na Musonda kwa dakika 90!
Nyie....! Hawaogopi?
ADVERTISE HERE