Winga Bernard Morrison amerejea nchini kuendelea na majukumu yake katika kikosi cha Yanga
Morrison alipewa ruhusu na uongozi wa Yanga kurejea kwao Ghana mwishoni mwa mwaka 2022 kushughulikia matatizo ya kifamilia
Morrison ambaye anafahamika kutokana na 'utukutu' wake, aliibua mjadala baada ya kuchelewa kujiunga na wenzake kambini akikosa mechi ya ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc juzi
Jana Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi aliwatahadharisha wachezaji wa timu hiyo kuwa hatawapa nafasi wachezaji ambao hawatazingatia ratiba ya timu
Nabi alisisitiza kuwa hakuna mchezaji mkubwa kuliko Yanga, na kuwa hataangalia majina ya wachezaji na hatajali kama wachezaji hao wanapendwa sana na mashabiki
ADVERTISE HERE