Mlinzi mpya wa Yanga Mamadou Doumbia anatarajiwa kutua nchini wakati wowote kuungana na wenzake baada ya kuondoka nchini Algeria alikokuwa akishiriki michuano ya CHAN
Doumbia ni nahodha wa timu ya Taifa ya Mali na alitarajiwa kuiongoza timu hiyo kwenye michuano ya CHAN inayohusisha wachezaji wa ndani
Baada ya kukamilisha usajili wake na Yanga ni wazi Doumbia amekosa sifa ya kuendelea kushiriki michuano hiyo kwa sababu hachezi tena nchini Mali
Mali ilicheza mchezo wake wa kwanza juzi Januari 16 dhidi ya Mauritania na kutoka sare ya mabao 3-3, huku Doumbia akikosekana katika mchezo huo.
Nyota huyo anatarajiwa kutua nchini wakati wowote kujiunga na wenzake wanaoendelea na mazoezi Avic Town kujiandaa na mechi za ligi kuu, kombe la FA na hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika