Wapinzani wa Yanga kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Barani Afrika, Township Rollers leo Jumatatu walikuwa dimbani kuchuana na BDF XI kwenye mchezo wa ligi kuu ya Botswana.
Mtanzania Rashidi Mandawa anakipiga katika timu hiyo BDF XI na leo amewalaza na viatu Township Rollers baada ya kupiga hat-trik kuiwezesha BDF XI kushinda kwa mabao 3-1.
Mandawa amefunga mabao 11 katika ligi kuu ya Botswana akiwa amecheza michezo 16.
Tayari viongozi wa Township Rollers wako nchini kuandaa mazingira ya kikosi chao kinachotarajiwa kuwasili baada ya mchezo huo.
Aidha, baada ya kuahirishwa mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, Yanga inatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam punde baada ya mchezo wake dhidi ya Ndanda FC.
March 06, Yanga itakuwa mwenyeji wa Township Rollers kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika, raundi ya kwanza.

ADVERTISE HERE