Kamwe aja na hesabu ya mechi nane za ubingwa Ligi Kuu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jan 2023
Kamwe aja na hesabu ya mechi nane za ubingwa Ligi Kuu

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wanahitaji kushinda mechi nane zinazofuatia kwenye ligi ili kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa pili mfululizo

Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kuiunga mkono timu yao katika mechi zilizobaki ili kuhakikisha wanatimiza malengo yao

"Kama tutashinda mechi nane mfululizo kuanzia mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, basi tutatwaa ubingwa. Kama tulihesabu 'unbeaten' mpaka zikafika 49, kuanzia Jumatatu tutaanza kuhesabu mechi nane zitakazotupa ubingwa"

"Tuna nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa kwani mechi nyingi tutacheza katika uwanja wetu wa nyumbani (Benjamin Mkapa Stadium) hivyo kila shabiki wa Yanga anapaswa kuhakikisha ananunua tiketi mapema kuwapa hamasa wachezaji wetu katika mechi hizi"

"Hatupaswi kuwaachia kina Mayele na Musonda pekee, nasi tunapaswa kutimiza wajibu wetu kwa kujitokeza kwa wingi katika mechi zetu ili kuhakikisha tunatimiza jambo letu," alisema Kamwe

Hesabu ya mechi nane itaanza Jumatatu wakati Yanga itakaposhuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Ruvu SHooting katika mchezo utakaopigwa saa 1 usiku

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
53m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’