Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema baada ya usajili wa dirisha dogo, kikosi chake sasa kimekamilika
Yanga imeongeza wachezaji wanne katika dirisha dogo ambao ni Metacha Mnata, Mamadou Doumbia, Mudathir Yahya na Kennedy Musonda
Nabi amesema kama wachezaji wake wote watakuwa 'fit', basi yeye na benchi lake la ufundi watakuwa na kazi ya kupanga kikosi kwani wamesheheni wachezaji bora katika kila eneo
"Ni timu bora kabisa tuliyonayo, kuwa na kundi la wachezaji bora kama hawa ni presha kubwa kwetu kama kocha kuhakikisha kila mchezaji anayekuwa na afya njema na yuko fiti kuhakikisha anacheza"
"Nawapongeza sana viongozi kuanza na mfadhili wetu Ghalib Said na Rais wetu na viongozi wenzake kwa kuunda timu kama hii ambayo kwanza ni gharama kubwa kupata watu bora kama hawa na kuwatunza, naona mambo mengi sio kitu rahisi"
"Kila mchezaji sasa anatakiwa kujiandaa kutoa mchango wake, tuna mechi nyingi za mashindano, ukiangalia tuna mechi zisizopungua 21 katika mashindano yote kila mchezaji anatakiwa kuongeza ushindani kuanzia mazoezini mpaka kwenye mechi," alisema Nabi