Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema kesho kabla ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting, watamtambulisha kwa mashabiki beki mpya wa timu hiyo Mamadou Doumbia
Doumbia ametua Yanga akitokea klabu ya Stade Malien, mabingwa wa ligi kuu ya Mali. Alikuwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Mali kinachoshiriki michuano ya CHAN huko Algeria
Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi dimba la Benjamin Mkapa siku ya kesho kumkaribisha beki huyo kisiki
Aidha, Kamwe amesema mkakati wa kushinda mechi nane mfululizo wanauanza dhidi ya Ruvu Shooting
ADVERTISE HERE