Kiungo Khalid Aucho hatarajiwi sehemu ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting leo akiendelea kuimarika baada ya kupona majeraha
Aucho amewatakia kila la kheri wachezaji wenzake katika mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 1 usiku
Kiungo huyo wa Kimataifa kutoka Uganda huenda akarejea uwanjani kwenye mchezo utakaofuata kombe la FA dhidi ya Rhino Rangers utakaopigwa January 27
Mwezi February hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho inatarajiwa kuanza ambapo February 12 Yanga itasafiri nchini Tunisia kuikabili US Monastir na kisha kurejea Tanzania kuikabili TP Mazembe, February 19
Aucho amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Yanga hivi karibuni akisaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Yanga
Ni moja ya silaha muhimu ya Yanga kuelekea hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho