Bao la kujifunga Mpoki Mwakanyuki kwenye dakika ya 33 limetosha kuihakikishia Yanga alama tatu muhimu katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Ulikuwa mchezo ambao vijana wa Ruvu Shooting walicheza kwa nidhamu kubwa katika ulinzi, Yanga haikutengeneza nafasi nyingi
Jesus Moloko alipoteza nafasi pekee adimu kwenye kipindi cha kwanza huku mlinda lango wa Ruvu akifanikiwa kuokoa mipira miwili ya kichwa kutoka kwa Fiston Mayele
Alama tatu muhimu zimewaimarisha Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 56, alama sita mbele ya Simba inayoshika nafasi ya pili
Mchezo unaofuata ni kombe la FA dhidi ya Rhino Rangers ambao utapigwa Januari 27-29 katika uwanja wa Benjamin Mkapa



ADVERTISE HERE