Doumbia anawasubiri Rhino Rangers

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jan 2023
Doumbia anawasubiri Rhino Rangers

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema beki mpya wa timu hiyo Mamadou Doumbia hakuweza kutumika katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting jana kwa kuwa hakufanya mazoezi na wachezaji wenzake

Kamwe amesema licha ya beki huyo kuwa 'fit' akitokea Algeria alikokuwa na timu ya Taifa ya Mali, benchi la ufundi limehitaji kumpa muda zaidi kwenye kiwanja cha mazoezi ili afahamu mbinu na utamaduni wa Yanga

"Doumbia aliwasili nchini Jumamosi usiku, hakuweza kufanya mazoezi siku iliyofuata kwa sababu alikuwa amechoka sana. Pamoja na kuwa yuko fit, benchi la ufundi liliona hakuna sababu ya beki huyo kuharakisha kumtumia"

"Timu yetu haikuwa na changamoto kwenye eneo la ulinzi kuelekea mchezo dhidi ya Ruvu Shooting. Naamini atakuwa na muda mzuri wa kufanya mazoezi na wenzake kuelekea mchezo wa kombe la FA dhidi ya Rhino Rangers siku ya Jumapili"

"Pengine Wananchi wataweza kumshuhudia katika mchezo huo," alisema Kamwe

Katika hatua nyingine, Kamwe amesema mshambuliaji Kennedy Musonda yuko fiti licha ya kuonekana anachechemea wakati akitolewa katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting jana

Kamwe amesema taarifa ya daktari wa Yanga imethibitisha kuwa Musonda hakuumia bali alipata mstuko wa misuli tu, yuko imara kutumika katika mechi zinazofuata

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
10h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
18h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’