Yanga bado haijasahaulika nchini Tunisia kutokana kile walichowafanyia Club Africain kwenye hatua ya mtoano michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Ushindi wa bao 1-0 ambao Yanga waliupata nchini humo dhidi ya Club Africain, uliwahakikishia Wananchi kutinga hatua ya makundi ya Shirikisho
Yanga inakwenda tena Tunisia kucheza mechi ya kwanza ya hatua ya makundi kombe la Shirikisho dhidi ya US Monastir, mchezo ambao utapigwa Februari 12
Ni wazi wakati huu Yanga watakumbana na upinzani mkali kutoka kwa Monastir ambao ni vinara wa kundi B ligi kuu ya Tunisia
Ushindi waliopata dhidi ya Club Africain umefanya mchezo huo kuwa gumzo kwani Watunisia wengi waliufahamu ubora wa Yanga baada ya mchezo dhidi ya Club Africain
Taarifa za ndani zinadokeza kuwa mashushushu wa US Monastir wako nchini kuichunguza Yanga, hii ni dalili ya hofu waliyonayo
Yanga inaendelea na mazoezi Avic Town kujiandaa na mchezo ambao utatanguliwa na mechi mbili muhimu, kombe la FA dhidi ya Rhino Rangers (Jan 29) na Ligi Kuu dhidi ya Namungo Fc (Feb 04) mechi zote zikitarajiwa kupigwa uwanja wa Benjamin Mkapa