Mapema leo, kocha mkuu wa Al Hilal Florent Ibenge alimtembelea mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele
Ibenge alikuwa kocha wa Mayele katika klabu ya AS Vita ambayo pia ilikuwa na nyota wengine wa Yanga Djuma Shaban, Joyce Lomalisa, Yannick Bangala, Jesus Moloko na Tuisila Kisinda
Ibenge yuko nchini na klabu ya Al Hilal ambayo imeweka kambi ya siku 10 kujiandaa na mechi za ligi ya mabingwa
Al Hilal ndio waliwaondosha Yanga raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1 baada ya ushindi wa bao 1-0 waliopata Sudan wakati mchezo uliopigwa jijini Dar es salaam ukimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Mayele alifunga bao pekee la Yanga katika mchezo huo, staili yake ya 'kutetema' inaonekana kumkosha kocha wake huyo wa zamani


ADVERTISE HERE