Burudani ya Wananchi inarejea hapo kesho katika uwanja wa Benjamin Mkapa, mabingwa kombe la FA, Yanga wakishuka uwanjani kupepetana na Rhino Rangers katika mchezo wa raundi ya tatu ya michuano hiyo
Huu ni msimu mwingine ambao Yanga imedhamiria kushinda mataji yote ya ndani kama walivyofanya msimu uliopita
Walianza na Ngao ya Jamii mwanzoni mwa msimu, wako kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC zikiwa zimesalia mechi 9 na leo wanawania nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora kombe la FA
Jambo moja la uhakika ni kuwa mechi hii haitakuwa nyepesi, Rhino Rangers kutoka mkoani Tabora wana kawaida ya kushangaza wengi pale wanapocheza na timu kubwa
Hata hivyo wanakwenda kukutana na Yanga ambayo imekuwa 'serious' sana, ikifanya maandalizi makubwa kuelekea hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Yanga itatumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi yake kuelekea mechi za CAF
Mchezo utapigwa saa 1 usiku