Yanga imetinga hatua ya 16 bora kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Rhino Rangers
Kennedy Musonda leo ameanza kuwafunga midomo wale walioanza ukosoaji akiweka kambani mabao mawili
Ulikuwa mchezo wa upande mmoja kwa muda mwingi pengine Yanga ilistahili kufunga mabao mengi zaidi kwa idadi ya nafasi walizotengeneza
Mabao mengine yalifungwa na Stephane Aziz Ki, Dickson Ambundo, Farid Mussa, Yannick Bangala na David Bryson huku Clement Mzize akikosa mkwaju wa penati
Yanga sasa itacheza na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora




ADVERTISE HERE