Stephane Aziz Ki kwa sasa ameamua miguu yake iwafunge midomo wale wakosoaji wake
Aziz Ki amekuwa na mfululizo wa kiwango bora katika mechi za hivi karibuni ambazo ameshiriki
Baada ya Feisal Salum kujiengua kwenye kikosi cha Yanga, wapo walioamini Yanga ingetetereka kwa kumkosa fundi huyo mahiri wa kupiga mashuti makali
Aziz Ki amezima kabisa mijadala yote vijiweni, kiuhalisia ameonyesha yeye ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa
Yeye ni mchezaji wa aina yake, kumfananisha na yeyote ndani ya ligi kuu ya NBC ni kumkosea heshima
Huyu ni mchezaji wa thamani kubwa! Anachezesha timu, anatoa pasi za mabao, anafunga na zaidi anawapa burudani mashabiki wa Yanga
Ki sio mchezaji wa kubahatisha, huyu ni fundi kwelikweli, mchezaji wa daraja la juu kabisa
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said anastahili pongezi kwa kufanikiwa kumleta Aziz Ki Tanzania