Kampuni ya kutengeneza vifaa vya Umeme, Haier imesaini mkataba wa kuidhamini Yanga kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Akizungumza leo katika hafla ya kusainiwa makubaliano hayo iliyofanyika Hotel ya Serena jijini Dar es salaam, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema mkataba huo wa muda mfupi una thamani ya Tsh Bilioni 1.5
Hata hivyo Hersi amesema kampuni ya Sportpesa itaendelea kuwa Mdhamini Mkuu wa Yanga kwa kipindi cha miaka mitano, Haier itaonekana kwenye jezi katika mechi za CAF tu kwa kuwa Mdhamini Mkuu wa michuano ya CAF ni 1xBet ambayo huduma anayotoa inafanana na SportPesa
Yanga inazindua jezi rasmi kwa ajili michuano ya CAF ambazo kampuni ya Haier itakaa sehemu ya kifuani badala ya Sportpesa
ADVERTISE HERE