Mashabiki wa Yanga watakuwa na furaha kusikia kiungo wao mahiri Khalid Aucho amerejea kikosini baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje ya uwanja kwa wiki kadhaa
Mara ya mwisho Aucho aliitumikia Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc uliopigwa Disemba 23 na amekosa mechi nne dhidi ya Mtibwa Sugar, Ihefu Fc, RUvu Shooting na Rhino Rangers
Hakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichoshiriki michuano ya kombe la Mapinduzi akiwa miongozi wa wachezaji waliopewa mapumziko
Alipata majeraha wakati Yanga lliporejea mazoezini baada ya michuano ya kombe la Mapinduzi
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kurejea kwa Aucho ni habari njema kwa kikosi chake
"Nimefurahi kuona kikosi changu kikiwa imara kutokana na uwepo wa baadhi ya wachezaji ambao walikosekana katika michezo iliyopita kwa ajili ya majeraha"
"Kati ya hao ni Aucho ambaye amepona majeraha yake yaliyomsababisha aikose michezo iliyopita," alisema Nabi
Mwishoni mwa wiki hii (Jumamosi) Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Namungo Fc katika mchezo wa ligi kuu