Ni wazi mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra anakwenda kutwaa tuzo ya kipa bora wa ligi kuu kwa msimu wa pili mfululizo
Diarra jana alihesabu cleansheet ya 13 katika ushindi wa mabao 2-0 ambao Yanga walipata dhidi ya Namungo FC
Msimu huu Diarra ameruhusu mabao tisa tu akimuacha mbali mshindani wake Aishi Manula wa Simba ambaye amefungwa mabao 12 huku akiwa na Cleansheet tisa
Wengi wanajiuliza kwa nini zile takwimu za cleansheet siku hizi hazitolewi tena baada ya Diarra kushika usukani?
Lakini habari ziwafikie, huyu Diarra ni kipa bora, hahitaji watu kumpigia kampeni mitandaoni aonekane ni bora
Ukitaka kujua ubora wa Diarra nenda kamuangalie uwanjani, halafu pia ukitaka ujue hao makipa wanaopigiwa kampeni sio bora basi we kawaangalie uwanjani!
ADVERTISE HERE