Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele anahitaji kufunga bao moja tu kwenye ligi ili kufikia rekodi yake ya mabao 16 aliyofikia msimu uliopita
Mayele amepania kuibuka mfungaji bora msimu huu akiwa na mechi nane za kufanikisha hilo
Kama ilivyo kwa Mayele, mlinda lango Djigui Diarra nae anawania kuvunja rekodi yake ya cleansheet 15 aliyoweka msimu uliopita
Diarra ana cleansheet 13 katika mechi 22, anahitaji cleansheet 2 tu kuifikia rekodi yake ya msimu uliopita
Wakati Mayele akiongoza mbio za ufungaji bora akiwa na mabao 15 tofauti ya mabao 5 dhidi ya Moses Phiri na Saido Ntibazonkiza wa Simba, Diarra nae anaongoza kwa tofauti ya cleansheet 3 dhidi ya Aishi Manula wa Simba mwenye cleansheet 10
ADVERTISE HERE