Yanga inaondoka leo jijini Dar es salaam majira ya saa 9 kuelekea Tunisia kupitia Dubai ambapo kikosi kitawasili Dubai majira ya saa ya 3:50 usiku
Kesho asubuhi saa 2:40 Yanga itaondoka Dubai kuelekea Tunis tayari kwa mchezo dhidi ya Monastir
Mchezo utapigwa katika dimba la Stade Olympique Hammadi Agrebi Jumapili Februari 12 kwa kuwa uwanja wa Monastir haukukidhi vigezo vya CAF
Uwanja wa Olympique Hammadi Agrebi ndipo Yanga ilishinda dhidi ya Club Africain
Yanga inaondoka na wachezaji 25 akiwemo mlinda lango Aboutwalib Mshery ambaye anakwenda Tunisia kwa ajili ya matibabu
Viongozi tisa wako kwenye msafara huo ambapo Mkuu wa msafara ni Seif Gulamali kwa upande wa Yanga
Kocha Nasreddine Nabi tayari ametangulia Tunisia
ADVERTISE HERE