Louis Houngnandande (37) raia wa Benin anatarajiwa kuwa mwamuzi wa kati wa mchezo kati ya US Monastir ya Tunisia dhidi ya Yanga ya Tanzania ambao utapigwa Jumapili, Februari 12 Stade Olympique Hammadi Agrebi
Mwamuzi huyo atasaidiwa na waamuzi wengine kutoa Benin ambao ni Eric Ayimavo, Koudogbo Kougbembe na mwamuzi wa akiba ni Dedjinnanchi Ahomlanto
Mara nyingi mechi za ugenini hasa kwa Mataifa ya Arabuni huwa na maamuzi ya kustaajabisha
Hata hivyo kama Yanga itakuwa na nidhamu ile waliyokuwa nayo kwenye mchezo dhidi ya Club Africain, hakutakuwa na namna, Monastir wanaweza kunufaika na mwamuzi huyo ambae ana sifa ya kumwaga kadi kama njugu
Habari njema kwa Yanga ni mchezo kupigwa Olympique Hammadi Agrebi uwanja ambao hata US Monastir watakuwa kama wageni baada ya CAF kuwagomea kutumia uwanja wao wa Monastir baada ya kukosa viezo