FT : Ndanda 1-2 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Mar 2018
FT : Ndanda 1-2 Yanga
Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wamewapa raha mashabiki wao wa mkoa wa Mtwara na Tanzania kwa ujumla baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ndanda FC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 19, uliopigwa kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Kabla ya mchezo wa leo, Yanga haikuwa imewahi kupata ushindi(hata kufunga bao) dhidi ya Ndanda katika dimba hilo la Nangwanda.

Aidha, idadi kubwa ya mashabiki wa Yanga wamejitokeza kwa wingi kuipa sapori timu yao iliyokuwa inasaka ushindi wake wa kwanza katika uwanja wa Nangwanda.



Ikicheza kwa tahadhari kubwa Yanga ilihesabu bao la kuongoza kwenye dakika ya sita mfungaji akiwa Pius Buswita aliyewahi krosi ya Hassani Kessy iliyowagonga walinzi wa Ndanda na mpira kuzagaa tu langoni.

Hassani Kessy akaifungia Yanga bao la pili kwenye dakika ya 29 akipiga shuti nje kidogo ya 18 baada ya kuwachambua walinzi wa Ndanda FC.

Ndanda FC ilitawala sehemu kubwa ya mchezo lakini walikosa mbinu ya kufunga bao.

Kwenye dakika ya 33 nusura Emanuel Martini aifungie Yanga bao la tatu lakini alichelewa kufanya maamuzi na kuanguka kabla mlinda lango wa Ndanda hajauwahi mpira na kuudaka.

Kwenye dakika ya 38 Yanga ilipata mkwaju wa penati baada ya mshambuliaji wa Ndanda Zabron kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Hata hivyo kiungo Papy Tshishimbi alishindwa kuukwamisha mpira huo wa adhabu kubwa baada ya mlinda lango wa Ndanda FC kuudaka.

Wakati wa mapumziko Yanga ilimtoa kiungo Papi Tshishimbi aliyeonekana kuchechemea mwishoni mwa kipindi cha kwanza na nafasi yake kuchukuliwa na Geofrey Mwashiuya.

Ndanda ilirejea kwa kasi kwenye kipindi cha pili na ilijipatia bao la kufutia machozi dakika moja tu tangu kuanza kwa kipindi hicho baada ya pasi ya Mrisho Ngassa kumpita mlinda lango wa Yanga Youthe Rostand na kumkuta Nasorro Kapama aliyekwamisha mpira wavuni.

Ndanda ilitawala mchezo muda mwingi wa kipindi cha pili ikisaka bao la kusawazisha lakini uimara wa safu ya ulinzi ya Yanga uliwezesha timu hiyo kuibuka na ushindi muhimu.

Matokeo hayo yameifanya Yanga ijiimarishe nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 40 ikiendelea kuwa nyuma ya Simba kwa tofauti ya alama tano.

Yanga imekamilisha ratiba yake ngumu kwa mafanikio makubwa baada ya kucheza michezo mitatu katika kipindi cha siku saba.

Sasa inarejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers unaopigwa March 06, 2018.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’