Kikosi cha Yanga kimeweka kambi katika Hoteli ya Kimataifa yenye nyota tano, Golden Tulip katikati ya jiji la Tunis
Yanga ilitua Tunisia jana na moja kwa moja kuingia kambini kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya US Monastir ambao utapigwa Jumapili, Februari 12
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wameweka kambi katika Hoteli ileile ambayo walikaa walipotua Tunisia mwaka jana kuikabili Club Africain
Amesema wamepata mazingira mazuri kwa ajili ya maandalizi yao akiwataka wapenzi, wanachama na mashabiki wa Yanga kuiombea timu yao ili kuhakikisha wanaondoka na ushindi siku ya Jumapili
Baada ya kutua jana, usiku wachezaji walifanya mazoezi maalum ya 'recovery' kuondoa uchovu wa safari ya siku mbili. Program za mazoezi zitaanza rasmi leo
Hali ya hewa ya Tunisia ni baridi kali hivyo uongozi wa Yanga umefanya uamuzi sahihi kutua nchini humo mapema kwani wachezaji watakuwa na siku tatu kuzoea hali hiyo