Uongozi wa Yanga umefanya uamuzi sahihi kuipeleka timu mapema Tunisia kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya US Monastir
Mchezo huo utapigwa siku ya Jumapili Februari 12 majira ya saa 1 usiku kwa saa za Tanzania
Hali ya hewa ndani ya Jiji la Tunis ambapo mchezo huo utapigwa ni baridi kali
Siku tatu za mazoezi zitatosha kwa wachezaji kuzoea hali hiyo na kuwa tayari kwa mchezo siku ya Jumapili
Hali ya hewa inashuka mpaka nyuzi joto 9 wakati wa jioni
Kikosi cha Yanga kinaendelea na maandalizi yake kuelekea mchezo huo





ADVERTISE HERE