Nabi anaandaa mbinu za kuimaliza US Monastir

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Feb 2023
Nabi anaandaa mbinu za kuimaliza US Monastir

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alikuwepo Stade Ahmed Khouaja, mjini Tunis juzi akishuhudia mchezo wa Ligi Kuu kati ya wapinzani wao US Monastir wakiwa ugenini dhidi ya Rejiche, ambapo walishinda 2-0, mabao yake yakifungwa na Idrissa Mhirsi dakika 10 na Bassam Deli dakika ya 30

Nabi pia alifanikiwa kushuhudia mchezo mwingine kabla ya huo kwenye Ligi wakati Monastir walipofungwa bao 1-0 na Ben Guerdan kwenye uwanja wa Mustapha Ben Jannet.

Yanga watakuwa ugenini kusaka pointi tatu muhimu katika mchezo wao huo utakaopigwa, Uwanja wa Olympique Hammadi Agrebi, katika mji huo mkuu wa Tunisia.

Profesa Nabi amebainisha kupata muda mzuri wa kuwatazama wapinzani wao Monastir katika michezo miwili waliyocheza kwenye ligi hiyo na kuona ubora na madhaifu yao.

Alisema amewaona wachezaji hatari ambao wanatakiwa kuwachunga na sehemu gani wako bora na wataingia katika mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi kwa tahadhari kubwa.

"Tumeona ubora wa kikosi cha wapinzani wetu kwa kushuhudia michezo yote miwili ya ligi kuu nchini humu, wachezaji gani ni hatari na wanaotakiwa kuchungwa tunapokutana nao"

"Tumefanya maandalizi mazuri tunatambua mchezo utakuwa wa ushindani mkubwa kwa sababu tuko ugenini na tunahitaji kupata alama katika mchezo wetu huo wa kwanza katika hatua ya makundi," alisema Nabi

Yanga imejichimbia Hotel ya Golden Tulip tangu walipowasili Tunisia juzi leo wakiingia siku ya tatu ya maandalizi yao

IPP Media

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
26m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
44m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
50m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’