Tuache lawama zisizo na msingi kwa Rostand

Muungwana wa Yanga By Muungwana wa Yanga
β€’
1 Mar 2018
Tuache lawama zisizo na msingi kwa Rostand
Kwa mtazamo wangu nadhani mlinda lango Youthe Rostand katika mchezo wa leo dhidi ya Ndanda FC amefanya vizuri.

Yapo makosa kadhaa aliyokuwa akifanya kama mchezaji mwingine lakini alijisahihisha kwa haraka.

Sidhani kama anastahili kulaumiwa kwa bao la Ndanda lililofungwa na Nasoro Kapama kwenye sekunde ya 35 kipindi cha pili.

Wachezaji wote wa Yanga walizembea katika ukabaji hivyo kupelekea kiungo Tsubi kuwa huru kupenyeza pasi kwa Mrisho Ngassa ambaye tayari alikuwa amemuacha nyuma beki Hassani Kessy.

Ngassa ni mchezaji wa Kimataifa, kubaki yeye pekee na kipa ni nadra sana kufanya makosa na hicho ndicho alichokifanya kwa kutoa pasi murua kwa mfungaji Kapama.

Hivyo wakati mwingine badala ya kulaumu wachezaji wetu ni vyema kuangalia matukio yanayopelekea kufungwa.

Ngassa alikuwa na mchezo mzuri na si ajabu kuchaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo.

Nadhani Ndanda wanastahili pongezi kwa bao lile kwani walitumia udhaifu wa wachezaji wa Yanga ambao walichelewa kuirudisha miili yao uwanjani na kujikuta wakishambuliwa kwa kushitukiza.

Na ndio maana baada ya kuingia kwa bao lile, umakini uliongezeka zaidi na Ndanda hawakufanikiwa kusawazisha licha ya kufanya majaribio mengi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’