Licha ya kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa US Monastir hapo jana, hesabu za Yanga katika mkakati wake wa kutiga robo fainali bado ziko salama
Jambo muhimu kwa Yanga ni kuhakikisha alama tisa za mechi tatu zitakazopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa hazidondoki
Ni kawaida kwa soka la Afrika, sio rahisi sana kushinda ugenini, Monastir wametumia vyema uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Yanga
Sasa ni zamu ya Yanga kutumia vyema uwanja wa nyumbani kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe siku ya Jumapili
Hautakuwa mchezo mwepesi lakini kwa ubora wa kikosi cha Yanga, uwezo wa kushinda mchezo huo ni mkubwa
TP Mazembe ndio vinara wa kundi D wao wakishinda mabao 3-1 dhidi ya Real Bamako nyumbani
Bamako wanashika mkia kundi D kwa sababu wao wameruhusu mabao mengi zaidi ingawa tofauti ya mabao kati yake na Yanga ni sawa (2)
Mechi ya Jumapili itatoa mwanga na hatma ya Yanga katika mpango wa kuvuka hatua ya makundi