Thierry Manzi amvutia Lwandamina

Yanga Damu By Yanga Damu
•
18 Jul 2017
Thierry Manzi amvutia Lwandamina
Beki wa kati wa timu ya Taifa ya Rwanda Thierry Manzi amemvutia kocha wa Yanga George Lwandamina na huenda uongozi wa mabingwa hao wa kihistoria Tanzania wakatia timu nchini Rwanda kuichukua sahihi yake.

Manzi alikuja na kikosi cha Rwanda na alionekana kwa mara ya kwanza na kocha huyo kwenye mchezo wa kufuzu kwa michuano ya CHAN kati ya Stars dhidi ya Rwanda Jumamosi iliyopita.

Katika mchezo huo Stars ililazimishwa sare ya bao 1-1 jijini Mwanza huku Manzi akimdhibiti hasa mshambuliaji wa Stars John Bocco 'Adebayor'.

Yanga inasaka beki wa kati kuziba nafasi ya Vicent Bossou ambaye klabu imeamua kuachana nae.

Kwa sasa kocha Lwandamina anaangalia viwango vya Henry Okoh kutoka Nigeria na Fenando Bongnyang kutoka Cameroon ambao wanafanya majaribio.

Lakini kama hawatamvutia Mwalimu basi huenda Thiery Manzi akapewa nafasi hiyo kutegemeana na matokeo ya majadiliano.

Pia Yanga inasaka mbadala wa winga Simon Msuva baada ya Difaa Al Jadida ya Morocco kumalizana na uongozi juu ya mchezaji huyo.

Issa Yahya ‘Akilimali’ winga mwenye kasi aliyerejea hivi karibuni kutoka masomoni nchini Uganda ni miongoni mwa wachezaji wanaofuatiliwa, imefahamika.

Mwingine anayetajwa kufuatiliwa na uongozi wa Yanga ni Haruna Chanongo, winga wa Mtibwa Sugar.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →