Beki kiraka wa Yanga Yannick Bangala amesema wachezaji wamejipanga na watahakikisha wanapata ushindi dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa pili hatua ya makundi michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Mchezo huo utapigwa Jumapili, Februari 19, uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 1 usiku
Bangala ambaye amewasili nchini na wachezaji wenzake leo wakitokea Tunisia, amesema wanaifahamu vyema klabu ya TP Mazembe
"Tunajua Mazembe inatokea Congo, ni timu kubwa yenye historia kubwa lakini hapa wanakuja kucheza kwetu, unapocheza nyumbani ni lazima ushinde tu"
"Kwa hiyo sisi tumejipanga kuhakikisha tunashinda mchezo huo. Tuko vizuri wala hatuna hofu yoyote kukabiliana nao," alisema Bangala
Bangala ni mmoja wa wachezaji waliowahi kuitumikia klabu ya AS Vita ambayo ni mpinzani mkubwa wa TP Mazembe kule DR Congo
Bangala ameshiriki mechi nyingi dhidi ya TP Mazembe akiwa na AS Vita
Wachezaji wengine ambao waliwahi kuitumikia AS Vita na kucheza mechi dhidi ya Mazembe ni Djuma Shabani, Joyce Lomalisa, Jesus Moloko, Tuisila Kisinda na Fiston Mayele