Kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe ambao utapigwa Jumapili, Februari 19, Wanachama na Mashabiki wa Yanga wana jambo lao pale Mbagala Zakiem kuanzia saa sita mchana
Ni katika tukio ambalo litawakutanisha Viongozi, Wapenzi, Wanachama, Mashabiki wa Yanga ikiwa ni sehemu ya shamrashamra na hamasa kuelekea mchezo dhidi ya TP Mazembe
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema Wachezaji wakiwa Avic Town watazungumza na Mashabiki wao kupitia 'Zoom'
Ni tukio la aina yake ambalo Mwananchi wa Mbagala na maeneo ya jirani hupaswi kulikosa
ADVERTISE HERE