Katika kuhakikisha mashabiki wanajitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa hapo kesho katika mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema kiingilio cha Mzunguuko kitabaki Tsh 3,000/-
Taarifa ya awali iliyotolewa na Yanga ilibainisha kuwa siku ya mchezo bei ya kiingilio Mzunguuko itakuwa Tsh 5,000/-
Hersi amesema katika kuhakikisha mashabiki wengi wanapata nafasi ya kushuhudia mchezo huo katika uwanja wa Benjamin Mkapa, wameamua kiingilio cha Mzunguuko kibaki Tsh 3,000/-
"Lengo letu ni kuona mashabiki wanakuja kwa wingi kuipa sapori timu kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe hivyo kiingilio cha Mzunguuko kitabaki Tsh 3,000/-," alisema Hersi
Viingilio vya majukwaa mengine vitabaki vilevile yaani VIP A ni Tsh 30,000/-, VIP B Tsh 20,000/- na VIP C ni Tsh 10,000/-
Hersi amewataka wachezaji wa Yanga pamoja na benchi la ufundi kuhakikisha wanawapa furaha mashabiki wao katika mchezo huo
"Nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto Yanga inataka ushindi, Fiston Mayele, Yannick Bangala, Stephane Aziz Ki, Djigui Diarra, Dickson Job, Joyce Lomalisa na wachezaji wengine wote tunawaambia Yanga inataka ushindi siku ya kesho," alisema Hersi wakati akizungumza na Wananchi baada ya jogging mapema leo