TP Mazembe wanafahamika kwa kucheza soka la nguvu nyingi na wakiwa ugenini hutumia zaidi mashambulizi ya kushitukiza
Bila shaka Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amechukua tahadhari zote kuwakabili siku ya leo kuhakikisha anarejesha furaha ya Wananchi
Kikosi cha Yanga kitakachoanza kinaweza kuwa mabadiliko kidogo kutoka kile kilichoanza mchezo dhidi ya US Monastir
Kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy' anakosekana leo akiuguliwa na mtoto wake, nafasi yake inatarajiwa kuzibwa na mchezaji mwingine
Yannicka Bangala leo huenda akarejea katika eneo la kiungo huku nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto anaweza kuanza sambamba na Dickson Job katika safu ya ulinzi
Pia kuna uwezekano Nabi leo akatumia washambuliaji wawili, Kennedy Musonda na Fiston Mayele mabadiliko ambayo yanaweza kushuhudia akibadili mfumo kutoka 4-2-3-1 kwenda 4-4-2
Eneo ambalo mashabiki wa Yanga wanasubiri kuona litakuwaje, ni washambuliaji wa pembeni
Tuisila Kisinda na Jesus Moloko walianza kwenye mchezo dhidi ya Monastir lakini Wananchi wanatamani kuona mabadiliko hasa katika nafasi ya Kisinda ambaye bado hajarejea katika ubora wake
Kinda Clement Mzize anapigiwa chapuo ya kuanza katika mchezo wa leo ambao Yanga inahitaji ushindi
Mzize ana kasi na anao uwezo wa kulazimisha mashambulizi kwa kulifuata lango tofauti na vile ambayo Kisinda hucheza
Hii ni mechi muhimu kwa Yanga kushinda na hakuna shaka, ITAWEZEKANA...!