Hassani Kessy siku za hivi karibuni amekuwa katika kiwango bora sana, hakika ndiye mchezaji bora wa kikosi cha Yanga wakati huu.
Kwa mara nyingine jana kwenye mchezo dhidi ya Ndanda FC Kessy amehusika kwenye mabao yote mawili ya Yanga. Alifunga bao la 'kideoni' huku krosi yake ikizaa bao jingine.
Katika mabao matano yaliyofungwa na Yanga karibuni, Kessy amehusika kwenye mabao manne.
Ukiacha mawili ya jana, Kessy alitengeneza bao moja kwenye mchezo dhidi ya Majimaji na hivyo hivyo kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya St Louis huko Shelisheli.
Hawa Washelisheli pia aliwavuruga kwenye mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam alisababisha adhabu ya penati ambayo chirwa alishindwa kuitumia kuifungia Yanga
Kessy ameongeza kujiamini na ni mmoja wa wachezaji wanaojituma sana katika kikosi cha Yanga.

ADVERTISE HERE