Ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe leo umeipandisha Yanga mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa kundi D
Yanga na TP Mazembe zote zina alama tatu zikiwa pia zimefanana uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa lakini Yanga inakuwa juu ya Mazembe kutokana na imepata ushindi dhidi ya Mazembe
Vigezo vinavyotumiwa na CAF kuamua msimamo timu zinapokuwa sawa kwa pointi wanaangalia timu ipi ilivuna alama nyingi timu hizo zilipokutana
Katika mchezo mwingine uliopigwa jana, Real Bamako walilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya US Monastir
Monastir wako kileleni mwa kundi D wakiwa na alama nne wakati Bamako wanaburuza mkia wakiwa na alama moja
Mchezo unaofuata kwa Yanga ni dhidi ya Real Bamako ambao utapigwa huko Mali Februari 26

ADVERTISE HERE