Kikosi cha Yanga Alfajiri ya kuamkia kesho Alhamisi kitaondoka nchini kuelea Mali kwa ajili ya mchezo wa raundi ya tatu kombe la Shirikisho dhidi ya Real Bamako
Wananchi wanakwenda Mali kuzisaka alama tatu muhimu katika mchezo utakaopigwa Jumapili, Februari 26
Yanga leo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC katika mchezo ambao kocha Nasreddine Nabi aliwapa mapumziko wachezaji wengi waliotumika katika mchezo dhidi ya TP Mazembe
Yanga inashika nafasi ya pili kundi D ikiwa na alama tatu sawa na TP Mazembe lakini Yanga iko juu ya Mazembe kwa sababu ya 'H2H'
ADVERTISE HERE