Nabi awatahadharisha wachezaji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Feb 2023
Nabi awatahadharisha wachezaji Yanga

Jana Yanga iliichapa KMC bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Kinda Clementi Mzize alifunga bao pekee la Yanga katika mchezo ambao Wananchi walijiongezea alama tatu ambazo zimezidi kuwaweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa baada ya kufikisha alama 62, alama nane zaidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili

Hata hivyo Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alieleza kutofurahishwa na kiwango cha baadhi ya wachezaji wake

Wakati akizungumza na wanahabari baada ya mchezo, Nabi alikwenda mbali zaidi kwa kusema mchezo wa jana ndio mchezo mbovu zaidi ambao ameshuhudia timu yake ikicheza tangu alipojiunga nayo

Alisema baadhi ya wachezaji hawako tayari kubadilika, na yeye hayuko tayari kuwa na wachezaji wa aina hiyo katika timu yake

"Hii ni mechi mbaya sana katika mechi zote ambazo toka nimeanza kufundisha Yanga, wachezaji wanaweza kusema ni uchovu ila sio sababu ambayo wanaweza kutumia wachezaji wengine"

"Kwa sababu wachezaji wamesajiliwa ili kucheza, hata wale ambao walikuwa hawachezi nao ni wachezaji ambao wanapopata nafasi ya kuvaa jezi ya Yanga ni lazima waoneshe kitu walichonacho"

"Unapewa nafasi unashindwa kuonesha! kuna wengine toka miaka miwili wajiunge Yanga kiwango ni kile kile. Wachezaji wengine hawabadiliki, hawaoneshi tofauti na wakiwekwa nje mara fulani hachezi mara mwingine anacheza"

"Ndio maana mechi ya leo wachezaji waliopewa nafasi hawakutaka kujituma kwa kuonesha kile ambacho wanacho, wachezaji ambao wamepewa nafasi ya kuvaa jezi na hawakujituma," alisema Nabi

Katika mchezo huo Nabi alifanya mabadiliko makubwa ya kikosi ambapo alianza na Diarra, Kibwana, Byson, Bacca, Mwamnyeto, Mauya, Kisinda, Sure Boy, Mzize, Aziz Ki na Ambundo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’