Tusikubali kutengenezewa hasira - Arafat

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Feb 2023
Tusikubali kutengenezewa hasira - Arafat

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amewataka Wanachama na Mashabiki kutoingia katika kinachoitwa hasira baada ya timu yao kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Real Bamako katika mchezo wa kombe la Shirikisho uliopigwa Bamako, Mali

Katika mchezo huo Yanga iliongoza mpaka dakika ya 90 kabla ya wapinzani wao kusawazisha bao kwenye dakika za lala salama

Arafat amesema kila mmoja alitamani kuona Yanga inaondoka na ushindi lakini hata alama moja waliyopata ugenini ina thamani kubwa

Amesema benchi la ufundi na wachezaji wameona makosa hayo yanayojirudia na hivyo wanastahili kupewa nafasi ili waweze kuyarekebisha

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Arafat ameandika;

"Sote tulitamani sana kuona tunashinda mchezo wa jana ugenini dhidi ya Real Bamako lakini haikuwa hivyo Mungu alitupangia kupata pointi moja ingawa tulikua na mchezo bora hata kutangulia kuongoza mchezo

Wananchi wenzangu tufunike kombe tusiingie kwenye mtego wa kutengenezewa hasira na wasiotupenda, haya sio matokeo mabaya kwetu kwani hakuna timu ambayo msimu huu inaweza kutubeza kwa ubora.

Wachezaji wetu na makocha wameona makosa na zaidi wameona aina ya mabao ambayo tumeruhusu yote ya makosa yanayojirudia.

Tuwape wachezaji wetu nafasi yao ya kujirekebisha wakati nasi viongozi tukitekeleza wajibu wetu nanyi mashabiki wetu niwaombe tekelezeni wajibu wenu uleule ili tushinde sote nyumbani tarehe 8 Machi 2023

Yapo mengi yalitukwaza kule kama timu ambayo sisi ambao hatukuwepo ni vigumu kuyajua, lakini wachezaji wetu na sisi viongozi tunajua njia za kupita kutumia nafasi ya sisi kuwa nyumbani pia, mtu kwao.

Twendeni Jumatano ya Tarehe 8 Machi 2023 tuendeleze furaha yetu kwani bado tuna nafasi kubwa ya kushinda na kufuzu kuliko kutolewa huu ni uamuzi wetu sote kwa kuamua kwenda pamoja.

Twendeni Wananchi wenzangu kwetu daima mbele nyuma ni mwiko"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’