Mlinzi wa kulia wa Yanga, Hassan Kessy huenda akapata fursa ya kuichezea Taifa Stars katika mchezo wa marudiano dhidi ya Rwanda Jumamosi ijayo.
Kessy aliyekuwa anasumbuliwa na matatizo ya misuli alinza mazoezi na kikosi cha Stars jana huku Shomari Kapombe akiondolewa kwenye kikosi kinachosafiri kesho Jumatano baada ya kupata majeraha.
Kapombe amerejeshwa Dar kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi kwenye kitengo cha mifupa Hospitali ya Muhimbili.
Licha ya kuitwa kwenye kikosi cha Stars inayonolewa na Salum Mayanga, Kessy hakuwa amepata nafasi ya kushuka dimbani tangu timu hiyo ilipokuwa inashiriki michuano ya Cosafa nchini Afrika Kusini.

ADVERTISE HERE