Alama sita zinaweza kutosha kwenda robo fainali

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Feb 2023
Alama sita zinaweza kutosha kwenda robo fainali

Yanga inaweza kujihakikishia tiketi ya kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika kama itashinda mechi mbili zinazofuata nyumbani

Machi 08 Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Real Bamako kisha kushuka tena katika uwanja huo kuikabili US Monastir Machi 19

Ikiwa nafasi ya pili kundi D na alama nne nyuma ya US Monastir yenye alama saba, kama Yanga itashinda mechi mbili zinazofuata itafikisha alama 10

Wakati Yanga ikichuana na Real Bamako Machi 08, TP Mazembe watakuwa Tunisia kumenyana na Monastir, hizi ndio mechi ambazo zinaweza kuamua hatma ya kundi mapema au la

TP Mazembe wanaweza kufikisha alama 12 kama watashinda mechi zote tatu zilizobaki, mechi mbili dhidi ya Monastir na Real Bamako wanacheza ugenini. Mechi ya kuhitimisha makundi watacheza na Yanga April 02 huko DR Congo

Ni wazi kama Mazembe hawatashinda dhidi ya Monastir iliyowachapa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa DR Congo, watairahisishia kazi Yanga kwa sababu kama watapoteza basi Yanga itatinga robo fainali kama itashinda mechi zake mbili zitakazopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Lakini pia hata kama Mazembe watapata matokeo ya sare, watakuwa na uwezo wa kufikisha alama 10 kama watashinda mechi mbili zitakazosalia na moja ya mechi hizo ni dhidi ya Yanga ambayo tayari iko mbele kutokana na rekodi ya H2H

Kimahesabu unaweza kusema bado timu zote zina nafasi ya kutinga robo fainali lakini Monastir na Yanga zina nafasi kubwa zaidi kwa sababu zimebakisha mechi mbili nyumbani wakati TP Mazembe na Real Bamako kila moja imebakisha mechi moja nyumbani

Hapa ndipo umuhimu wa alama sita za mechi mbili zitakazopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kwani zinaweza kutosha kuivusha Yanga robo fainali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’