March 08, siku ya Jumatano, ni maalum kwa Wananchi pale uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Real Bamako
Mechi kubwa, mechi ya heshima kwa Yanga, mechi ya kuisaka robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Pamoja na kushiriki mara nyingi kwenye michuano ya CAF pengine kuliko timu yoyote Tanzania, Yanga haikuwahi kuvuka hatua ya makundi
Lakini msimu huu dalili ni njema, alama sita kwenye michezo miwili inayopigwa dimba la Mkapa dhidi ya Real Bamako na US Monastir, zinaweza kutosha kuihakikishia Yanga kuvuka hatua hiyo
Kama hujakata tiketi bado basi fanya hivyo sasa, siku ya Jumatano dimba la Mkapa linapaswa kuwa full




ADVERTISE HERE