Wakati Yanga ikiendelea na maandalizi kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Real Bamako ambao utapigwa Jumatano, March 08 2023, habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni urejeo wa winga Benard Morrison ambaye ameanza mazoezi mepesi
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema baada ya Morrison kukosekana tangu mwishoni mwa Disemba 2022 akiwa ni majeruhi, mchezaji huyu ameanza mazoezi
"Nina habari njema kwa mashabiki wa Yanga, mchezaji wetu Bernard Morrison ameanza mazoezi mepesi mbioni kurejea katika majukumu yake baada ya kuwa nje kwa muda mrefu"
"Wachezaji wengine wanaendelea na maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Real Bamako, ari na morali yao iko juu kila mmoja ana matumaini tutashinda siku ya Jumatano," alisema Kamwe
Morrison amekuwa akisumbuliwa na jeraha la nyama za paja, jeraha ambalo alikuwa nalo tangu alipojiunga na Yanga
Kwa kutambua na kuthamini mchango wake kikosini, uongozi wa Yanga ulichukua jukumu la kumpa matibabu sahihi ili kuhakikisha anakuwa timamu na kuweza kutimiza majukumu yake ipasavyo
Morrison anaweza kushiriki mechi za mwisho hatua ya makundi dhidi ya US Monastir na TP Mazembe