Jumatano March 08 ni Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Katika siku hii pia Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Real Bamako katika mchezo wa raundi ya nne hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika
Kwa kutambua siku hii, Yanga ilialika Taasisi, Makampuni na Watu binafsi kujitolea kununua tiketi kuwazawadia Wanawake ili kuwapa fursa ya kushuhudia mchezo huo katika maadhimisho ya siku yao Maalum
Zaidi tiketi 2250 zimenunuliwa huku zoezi hilo likiendelea lengo likiwa kuwapa fursa Wanawake wengi kwenda kushuhudia mchezo huo muhimu ambao Yanga inahitaji kushinda
Walionunua tiketi kwa ajili ya Wanawake ni pamoja na Lampard Electronics (300), Bullet Force Security (100), CRDB Bank (100), Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Haji (100), Mjumbe Kamati ya Utendaji Yanga Makaga (150), Mjumbe Kamati ya Utendaji ya Yanga Munir Said (100), Mjumbe Kamati ya Utendaji Yanga Alex Ngai (100) na Omary Kimosa (100)
Wengine ni Crispo Hezron (100), Ibrahim Samwel (100), Ronas Wine (100), Kangaroo Insurance (100), FreeLance (300), Naibu Waziri Wizara ya Kilimo na Mh Anthony Mavunde (200), Jembe Energy (300)
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewashukuru wote waliojitolea kununua tiketi kwa ajili ya Kinamama huku akiwataka Mashabiki kuendelea kununua tiketi ili kuhakikisha uwanja wa Benjamin Mkapa unajaa siku ya Jumatano
Kamwe amesema siku ya kesho Jumanne, March 07 itakuwa maalum kwa ajili ya kununua tiketi ambapo Mawakala wa kukata tiketi watakuwepo Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani kwa ajili ya kuwahudumia Wananchi