Baada ya kupokea Maamuzi ya marejeo ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kuhusu suala la mchezaji Feisal Salum, klabu ya Yanga imemuandikia barua mchezaji huyo kumtaka aripoti kambini
Yanga imemtaka Feisal kuutumikia Mkataba wake kama mchezaji halali wa Yanga hadi Mei 30 2024
Yanga imebainisha kuwa tayari kumpokea Feisal na pia iko tayari kufanya majadiliano nae kwa ajili ya kuboresha maslahi yake
Lakini pia Yanga iko tayari kumruhusu Feisal aondoke kwa kuzingatia taratibu zilizoainishwa na TFF na FIFA
Kwa timu inayomuhitaji Feisal imekaribishwa kwenye meza ya majadiliano

ADVERTISE HERE