Matchday : Yanga vs Real Bamako, CAF CC, MD 4

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Mar 2023
Matchday : Yanga vs Real Bamako, CAF CC, MD 4

Leo majira ya saa 1 usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa, kikosi cha Yanga kitakuwa uwanjani kuikabili Real Bamako katika mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika

Ni mchezo wa raundi ya nne kundi D Yanga ikizihitaji alama zote tatu ili kuweka hai matumaini ya kutinga robo fainali

Ni mechi inayopigwa katika siku maalum, siku ya kuwaenzi Wanawake Duniani, Yanga imewaandalia zawadi kubwa katika siku hii

Baada ya kufanikiwa kuondoka na alama moja kule Mali, leo Yanga ina kazi moja tu, kuhakikisha inashinda ili kufikisha alama saba

Kwa Mkapa ni Full Shangwe leo, kwani kabla ya mchezo kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewataka Wananchi kuhakikisha wamekata tiketi zao mapema mpaka sasa tiketi za VIP A zikiwa zimemalizika

Kamwe amesema leo wachezaji wanahitaji kuona 'vibe' zaidi ya lile waliloshuhudia katika mchezo dhidi ya TP Mazembe ambayo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-1

Kama Yanga itashinda leo na TP Mazembe kupoteza nchini Tunisia dhidi ys US Monastir, basi Yanga itahitaji kushinda mchezo utakaofuata dhidi ya US Monastir ambao pia utapigwa dimba la Mkapa ili kufuzu robo fainali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’