Nabi ataja sababu ya kumtoa Aziz Ki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Mar 2023
Nabi ataja sababu ya kumtoa Aziz Ki

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema alilazimika kufanya mabadiliko ya kimbinu wakati wa mapumziko baada ya timu kupoteza muundo wake hasa baada ya kufunga bao la kuongoza

Nabi alitoa ufafanuzi huo baada ya sub ya Stephane Aziz Ki ambaye alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Khalid Aucho

"Tumepata matokeo mazuri tofauti na mechi iliyopita. Tunafurahia kama timu tumepambana kupata ushindi huu"

"Tumecheza na timu nzuri, kipindi cha pili ilibidi tubadilike, na tukacheza vizuri na mmeona tumepata ushindi"

"Sote tunafahamu uwezo na ubora wa Aziz Ki ila changamoto ni nidhamu ya kimbinu (tactical discpline) baada ya kufunga bao tulipoteza Kiungo chetu kwakuwa alikuwa hashuki kusaidia (track back) na sio yeye tu hata Mawinga hivyo ililazimu kuwatoa kurekebisha," alisema Nabi

Kuingia kwa Khalid Aucho na Jesus Moloko kulibadili taswira ya mchezo Yanga ikitawala safu ya kiungo pamoja na kutengeneza mashambulizi zaidi

Kuhusu changamoto ya kukosa mikwaju ya penati, Nabi amesema jambo hilo hawalifurahii na anaamini wachezaji watafanyia kazi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
47m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’